Sunday, December 27, 2009

LADY JAYDEE NA WATOTO SO NICE!!!
Special Pongezi kwako Lady Jaydee & Machozi Band

Ni nadra sana na adimu kwa wasanii wetu kukumbuka kuwa watoto pia wanastahili kupewa burudani na kukumbukwa kipindi cha sherehe,hii ki masoko ni kitu makini na muhimu maana unawajenga watoto na kuwapa image sahihi na kuwafanya wakue na wapende muziki wako.ni imani yangu wale watoto watakuwa wapenzi wa baadae wa Machozi band na wataendelea kuwa mabalozi wazuri wa bendi yako wakiwa mashuleni,nyumbani etc.

Sio tu kuongeza mashabiki bali ni kuongeza thamani ya bendi na kuwapa watoto haki yao ya msingi kukutanika na kupata burudani,nakupongeza sana na kukupa big up sana kwa idea yako maana ki ukweli watoto walifurahi sana na kupata burudani fresh.

Mungu akuzidishie maisha marefu na kukupa kheri katika yote,kwani maisha ni mapambano so aluta continua.


Best regards,

The Editor Mac Temba Jr

No comments: