Wednesday, January 28, 2009

D.G. ENTERTAINMENT BACK WITH KENNY ROLLINKampuni ya Dynamic Group Entertainment imeamua kuja kwa kasi mpya ikiwa na dhumuni la kusaidia wasanii wa hapa Tazania kujitangaza zaidi kupitia Video na matangazo ya bidhaa mbalimbali,Ujio huu ni pamoja na kuingia mkataba na Mtengenezaji chipukizi na mkali wa video Kenny Rollin aliyepata kuwa na kampuni kama Big Time Productions na Hartmann Productions...Ujio huu mpya wa Kenny chini ya Lebo hii ya Dynamic Group Entertainment yenye ofisi zake Sinza- Mori ni pamoja na maandalizi ya Video za msanii Joslin na wimbo wake unaotamba hivi sasa "One Day" uliotengenezwa na producer mkali wa Tongwe Records kijana Duke Tachez pamoja na single ijayo ya msanii Mr Blu aka Kabyser na wasanii wengine wengi...Kenny Rollin anasema alipokuwa kwa Hatmann Pro aliweza kutengeneza video mpya ya msanii Dully Sykess uitwao "Watasimuliwa" inayotamba katika stesheni mbalimbali za televisheni hapa Bongo.


So kwa wapenzi wote wa burudani kaeni mkao wa kula na kusubiri mambo makubwa kutoka kwa Kenny Rollin aka Key na Lebo hii mpya ya DYNAMIC GROUP ENTERTAINENT.
No comments: