Friday, January 30, 2009

MPYA TOKA KWA MUSTAFA HASSANALI!!!

MALKIA’ 2009 ONYESHO LA MAVAZI KUZINDULIWA

Mbunifu Maarufu wa mavazi Nchini Mustafa Hassanali anatarajia kufanya onyesho la mavazi la aina yake ya kuvutia kwa jina la ‘MALKIA’ siku ya JUMAMOSI TAREHE 7 FEBRUARI katika ukumbi wa LITTLE THEATRE iliopo kando na KANISA LA ST.PETERS katika barabara ya Haile Sellasie road.

Onyesho la ‘Malkia’ litaonyesha ubunifu mpya na wa kisasa zaidi wa mavazi ya harusi. Onyesho hili limedhaminiwa na Zain, Stella Artois na MotoMedia.

Mustafa Hassanali ni mbunifu maarufu aliyebobea. Kazi zake ni za ubunifu wa hali ya juu, nakshi ya aina ya kipekee ambayo haina upinzani katika dunia ya mavazi na mitindo hapa Tanzania.

Mustafa amefanikiwa kufanya maonyesho Nchi tofauti za Afrika pamoja na Europa hivyo kuweza kubuni mitindo yenye ubora na hadhi ya kimataifa na kuweza kuinua soko la mitindo na mavazi nchini.FOR IMMEDIATE RELEASE


CONTACT:
CONTACT PERSON: MUSTAFA HASSANALI
COMPANY NAME: MUSTAFA HASSANALI COUTURE
PHONE NUMBER: +255-76-7303880 /+255-78-4303880
EMAIL ADDRESS: media@mustafahassanali.net
WEBSITE URL: http://www.mustafahassanali.net/

No comments: