Wednesday, May 07, 2008

IM SORRY MY BLOG FANS!!!

Hello my blog fans!!!

Im so sorry kwa kuwa kimya sana kwa almost wiki mbili hivi...Nilipatwa na janga la moto nyumbani kwangu ambapo ni makao makuu ya blog hii,Tukio hili la moto lilitokea siku ya Jumatatu tarehe 28/04/2008 saa kumi jioni eneo la Shekilango Road Bamaga opposite na chuo cha Ustawi wa jamii...Tukio hilo lilisababishwa na hitilafu ya umeme wa Tanesco na kunisababishia hasara ya kubwa maana moto uliunguza kila kitu ndani ya nyumba ...Kwa kweli ilikuwa ni kitu kigumu kuamini ila mungu amenipa nguvu na ujasiri wa kukubaliana na yaliotokea na kuanza maisha mapya...Natoa shikurani kwa wote walioguswa na tatizo hili lililonipata na kwa niaba yangu na mchumba wangu Zhane napenda kuwashukuru wale wote waliotupa nguvu na kuonyesha upendo wa dhati kwetu naamimi mungu ni mwema na atawabariki sana.Salaam nyingi za Shukrani kwa Magumashi family chini ya uongozi wa Mh Danny Kiganga aka Danny Star kwa upendo wenu na bila kusahau kaka yangu Abdul Gwello na dada yangu jackie wa gwello kwa yote ... mungu awazidishie....

Nawaahidi mambo makubwa kutoka katika blog hii wakati huu najipanga na mdhamini wa blog yangu Director Gabby Makupa wa GRM Investment Ltd....Stay positive m amini Gods loves u so show love to each other...


With Love,

Edwin Mac Temba
Chief Editor of www.mactemba.blogspot.com
+255 715 000 890

2 comments:

Anonymous said...

Kaka kwanza pole na kama ulivyo sema mungu anatupenda na matokeo ya yote hayo apana apaswae kuabudiwa ila ni yeye mwingi wa rehema na naomba uamini kuwa kila linalo mfika mwanadamu yani hata ukijikwaa barabarani basi mungu alisha andika hilo akuna atakae weza kuepusha hilo ispokuwa yeye tu,na napenda nioyeshe hisia zangu mimi ni mdau mpya kabisa wa blog yako kwani siku niliyokutembelea kwa mara ya kwanza nilifurahi sana na kuapa kuitembelea kila siku lakini nikawa naona kimya nikajipa moyo huenda ndio utaratibu wako nikawa sichoki nikakutembelea kila siku mpaka hii leo nilipo kutana na habari za kuhuzunisha kweli zimenistua sana nachoweza kusema kuwa pole kaka kwa yaliyo kukuta yoite maqisha siku zote mlango mmoja ukifungwa mungu anakufungulia mwingine naamini utapata vitu vingi na vizuri kuliko hivyo vilivyo uungua. Mdau toka zenji

Anonymous said...

ohh pole sana kwa matatizo yaliokupata, usijali mungu yupo nawe,bila shaka atakusaidia utaendelea na maisha yako vizuri kama mwanzo ingawa si rahisi sana kupata vyote ulivyopoteza kwa mara moja but utafanikisha tu nakuombea baraka ufanikiwekila unachofikilia..ni mimi JAWA MARIRI SWEDEN.