Tuesday, April 01, 2008

MIMBA NA VIVAZI VYAKE!!!


Mimba ni ile hali ya mwanamke kuwa na mtoto tumboni mjamzito, ambaye nae ana mavazi yake rasmi ya kuvaa wakati huo ambao maarufu yanajulikana kama matenite.

Matenite ambayo yamezoeleka hapa kwetu ni gauni kubwa lililo pana haswa haswa likiwa la kitenge

Jamani kina dada tubadilike matenite si guo pana la kitenge pekee pali kuna mateniteya suruali, kapri, minisket kuna blauzi pia za mimba kibao kwa sasa

Na je utazitambuaje kama ikiwa ready made utaikuta kwenye lebo imeandikwa kabisa kuwa hili ni tenite au kama ni suruali, pensi ,kaptura,au sket utakuja juu tumboni kuna mpira au kuna mkanda ambao unaongezeka na kupunguzika kulingana na ukubwa wa tumbo.

Pia kuna blauzi ambazo zinakuwa zimeshonwa hadi chini ya matiti ndipo zikaja kuunganishwa na chini kuachiwa kulipa nafasi tumbo lisiweze banwa.THIS POST WRITTEN BY SHAMIM OF DARHOTWIRE.

No comments: