Tuesday, November 27, 2007

BONGO STAR SEARCH KWELI NI MKOMBOZI WA WASANII CHIPUKIZI???

Ni wakati mwingine tena msimu wa kumtafuta staa mwingine wa Bongo star search aka BSS wa mwaka 2008,ni jambo lisilofichika kuwa nia ni nzuri na maandalizi yanakwenda sawa katika zoezi lote la kumsaka staa mpya wa muziki hapa nchini kwetu Tanzania.

Kwangu mimi nina mtazamo ulio tofauti na wapenzi wengine wa shindano hili,ni mategemeo yangu kwa haya nitakayoyagusia utakubaliana na mimi kuwa ni mtazamo sahihi au waswahili wanasema mtazamo chanya,Naamini kuwa lengo la shindano la Bongo Star Search ni kumsaidia msanii chipukizi na ili hatimae kupata mafanikio katika sanaa ya muziki na wala sio kumpa gari na kumwacha njia panda,nilitumaini kuwa baada ya Jumanne Iddi kushinda na kupata gari angepata pia msaada wa mawazo na muelekeo wa ushauri wa kimuziki na ki masoko ili kupata mafanikio katika muziki.Sasa ni miezi tangu Jumanne Iddi apate ushindi na hakuna jipya juu yake,sioni mafanikio yeyote katika muziki wake zaidi ya kupata zawadi ya gari, nimesikia nyimbo kama mbili na kuona video yake na katika hili nashawishika kusema Benchmark Productions hawajafanikiwa kufikia malengo katika kumsaidia mshindi wa Bongo Star Search wa kwanza. Zawadi zilikuwa nzuri na za kutia motisha lakini mwisho wa siku lazima lengo litimie la kumsaidia msanii husika kupata mafanikio katika sanaa ya muziki na sio kumpata mshindi kioo ambaye baada ya mwaka mmoja anapotea kama upepo,Ni ukweli usiopingika kuwa tuna hazina ya wasanii chipukizi wengi tatizo ni malengo sahihi ya wadau,shindano la Bongo star Search lilitoa wasanii wengi wazuri kama Chiku Ketto aka BSS 05,Leah Muddy,Aboubakary Mzury na wengine wengi swali ni Wako wapi mastaa wa mwaka jana kama hao???je waandaaji wamewasaidia nini wale wa mwaka jana angalau kufikia malengo yao katika sanaa?Je baada ya shindano waandaaji hawakai chini na kufanya evaluation ya shindano lililopita na kupanga mikakati ya kuwasaidia angalau wale Top finalist wa BSS.Ni matumaini yangu kuwa waandaaji watabadili muelekeo ili kuleta maana halisi ya shindano hili,lisiwe ni shindano la kuwanufaisha waandaaji na kuwanyonya wasanii wachanga….Ni kweli BSS ni mkombozi wa wasanii wachanga au………

Mtazamo wangu ni huu ili kuleta maana halisi na kuwasaidia wasanii wetu wachanga ki ukweli na sio kuwatumia kibiashara.

1 comment:

Anonymous said...

Mdau,

Vichwa huwa vinatoka hata bila msaada.

Misaada ingekuwa deal basi Bongo kama taifa tungekuwa mbali sana ... maana tunamiminiwa misaada kila siku!

Msaada mzuri ni ule utakaojipa mwenyewe, sio wa kupewa.