Thursday, November 29, 2007

BIFU KATIKA MUZIKI WETU HUMSAIDIA NANI???
Kwa takribani mwaka mzima muziki wetu umetawaliwa na mizengwe mingi pamoja na magomvi kati ya wasanii na wasanii,ukiuliza wadau na wapenzi wenyewe wanasema ni" Bifu"Msemo huu umetokana na neno la kiingereza Beef,huu ni msemo wa kijinga na unaosababisha muziki wetu uzidi kudidimia chini siku hadi siku,sifikiri kama kuna msanii hata mmoja hapa kwetu ambaye bifu hizi zimemsaidia zaidi ya kumporomosha na kumpoteza katika ramani ya muziki wetu mifano imekuwa mingi na tumeyaona mengi ya kujifunza...Wasanii wengi wamegombana na hawaongei mpaka leo na kuongeza visasi kati yao,makundi mengi yamevunjika na muziki wetu umeendelea kuporomoka na kupoteza muelekeo…Wenzetu marekani bifu hutumika kuongeza mauzo ya santuri zao,tumejionea bifu nyingi kama ya The Game Vs 50 cents mwaka jana,na mwaka huu Kanye West Vs 50 Cents,wao hufanya malumbano hayo kibiashara ili kuvutia vyombo vya habari na lengo ni kuongeza mauzo ya kazi zao,lakini hapa kwetu bifu ni matusi na ngumi na mwisho hakuna yeyote anayejisaidia kuuza album yake sokoni zaidi,Je swali la kujiuliza ni kuwa Bifu chanzo chake ni nini?Bifu nyingi za hapa kwetu husababishwa na wasanii wachache wasiopenda kukosolewa na wasiopenda kuambiwa ukweli kuwa viwango vyao ni vidogo,nasikitishwa sana na msanii anayeanzisha bifu eti kisa kaambiwa Fulani kamfunika! suluhisho sio magomvi dawa ni kujipanga na kufanya kazi za uhakika ili uweze kukubalika.Je muziki wetu umefikia mahali pa kuleta ubaguzi wa ki- kanda?U mikoa?eti huyu wa Arusha mimi wa Dar?Ninavyojua mimi muziki hauhitaji mambo yote hayo zaidi ya kufanya kazi nzuri ili wapenzi wa muziki waweze kukukubali,Hata kama utatoka Nanjilinji au Mtwara maadamu unafanya kazi nzuri utakubalika na utaweza kupata mafanikio,Kwani kuzaliwa Dar kunampa msanii faida gani katika muziki au sanaa ya muziki???Ni ujinga kufanya kazi mbaya na kujisifu eti mimi nimezaliwa mjini! so what?.Miezi michache iliyopita nimepata taarifa ya bifu eti kati ya wasanii wa Hip hop wa Dar (Kikosi cha mizinga) na wenzao wa Arusha Nako 2 Nako soljas)...Kwa mtazamo wangu naona ni wivu tu a kitoto usiokuwa na malengo ya kuendeleza muziki wetu,haijifichi kusema kuwa Hip Hop yetu imeshikwa na wasanii wakali wenye kufanya kazi na wasiopenda bifu za kitoto kwasababu wana uwezo na wanafanya kazi na kutoongea sana wala kujisifia sana,Hip hop haitaki mambo mengi,kama wewe ni mkali utajulikana na hawezi mtu kukataa ukweli huo,Ni wakati wa wasanii wa Kikosi cha mizinga kukaa chini na kujipanga na hasa kujiuliza wanafanya bifu hizo ili wapate umaarufu au zinawasaidia kuuza kazi zao kama zipo sokoni???Sioni sababu ya wasanii wakali kama Joh Makini,Nako2Nako,Chid Benz,Prof Jay aka Jizze,Jay Mo,Fid Q,Ay,Mwana Fa kuchukiwa wakati wameshaweza kupenya na kuwa matawi ya kueleweka katika muziki wetu wa Bongo,Itakuwa jambo la ajabu kufanya kitu bila kuwa na malengo ya baadae,kwa maana bifu lazima iwe na maana la sivyo wanaopenda muziki watakuona wewe mwehu na huna mwelekeo na ndio itakuwa sababu ya wapenzi kuacha kununua na kusikiliza muziki wako.Ni jukumu la wasanii wote wachanga na wale ambao hawajaweza kupata mafanikio kupata ushauri toka kwa wale walioweza ili na wao waweze kupata mafanikio,Dr dre alimsaidia Eminem kupata mafanikio,Eminem kamsaidia 50 cents kupata mafanikio na kama haitoshi 50 cents kawasaidia Lloyd Banks,Tony Yayo na Young Bucks kupata mafanikio huu ndio mfumo mzuri wa sanaa na wala sio bifu,muziki wetu ni mchanga na ni wajibu wa wasanii wetu kufanya mambo ya msingi ili kuepuka malumbano ya kila siku,Mr 2 sugu alisababisha mpaka wazee waupende muziki huu lakini bifu zitasababisha wapenzi wa muziki huu kuuchukia na kuachana na muziki wetu.Tuamke na wasanii wafanye mambo ya msingi ili kukuza muziki wetu na wala sio kukuza bifu zao.

Wake up dawgs and keep Hip Hop Alive!!!

EDWIN MAC TEMBA


1 comment:

fnice said...

Hayo nikati ya mambo ambayo yanawafanya watu waseme...... "Hip hop is Dead wakati hip hop is not dead the game hip hop is just began"..... Washkaji let's take dis bongo flava to some next level.. one! FREDNICE -Birmingham, UK