Wednesday, May 05, 2010

Tip Top Connection 'Wanapika' Albamu Mpya


NYOTA wanne wa bongo flava wanaofanya kazi chini ya kundi la Tip Top Connection, muda si mrefu wanatarajiwa kuingia studio tayari kwa maandalizi ya kurekodi albamu yao ya pamoja.Wasanii hao nyota ni pamoja na Khadija Shaban ‘Keysha’, Ahmad Ally ‘Madee’, Harid Tunda ‘Tundaman’ na Kassim Mganga ‘Cassim’.

Akizungumza na mwandishi wa blobu hii kwa njia ya simu, Meneja wa Tip Top Connection, Babu Tale alisema kwamba, albamu hiyo itakuwa na nyimbo 10, ambapo zote wataimba kwa kushirikiana.

Tale alisema ili kuweka vionjo tofauti, nyimbo zitakazokuwemo katika albamu hiyo watazirekodi katika studio zaidi ya moja, zikiwamo Mj Records, Ngoma Records, Tongwe Records, Bongo Records na nyinginezo.

Aliongeza kuwa licha ya wasanii hao kuandaa albamu hiyo, haitaathiri matayarisho ya kazi zao, ambapo kila mmoja ataendelea kufanya kazi zake ikiwamo kurekodi nyimbo kwa ajili ya albamu yake.

Kwa sasa wasanii hao wanatikisa katika anga la muziki wa kizazi kipya kupitia vibao vyao walivyoachia hewani kila mmoja, ambapo Cassim anatamba na ‘Amore’, Tundaman anang’ara na ‘Hali yangu mbaya’, huku Madee akiwa na ‘Hakuna kuogopa Polisi’

No comments: