Saturday, February 20, 2010

MSEMA KWELI ALONGA KUHUSU KILI AWARDS


Ni juzi tu Kili Award imetangaza lengo lake la kuwapa tuzo wanamziki na bendi za mziki
nchini.
Lakini wimbi kubwa linaonekana kuvamia meza ya kamati ya Kili Award,kwani tayari malalamiko
kutoka kwa wadau na washabiki wa mziki nchini,wanadai kuwa katika uteuzi wa nani? apewe tuzo za Kili
kuna hewa ya ubaguzi,hewa hiyo ya ubaguzi inajipenyeza bila wanakamati kujua!!
Washabiki na wadau wamziki wanalalamika kwa nini? kamati ya Kili Award itambue mchango na kuwapa
tuzo hizo wanamziki wa nchi jirani kwa kigezo cha East African best artist,badala ya kuwapa wanamziki
wa tanzania walio nje ya nchi? ambao kazi zao na nyimbo zao zinafanya vizuri sana ndani na nje ya nchi,
isitoshe wanamziki wa tanzania na bendi zao walio nje ya nchi wamekuwa mambalozi wazuri wa kulitangaza
taifa katika njia ya mziki.
Wadau wanaendelea kulalamika kuwa hiwapo kamati ya Kili Award inaweza kuzitambua kazi za wanamziki
kutoka nchi jirani,kuna ugumu gani ? wa kuzitaambua kazi za wanamziki wa Tanzania walio nje ya nchi,
wakati mchango wao ni mkubwa kuliko wa wanamziki wa nchi jirani.
Moja katika ya watunzi na waimbaji wa kitanzania walio nje ni mwanamziki nyota Ebrahim Makunja aka
Kamanda Ras Ebby Makunja,anayeongoza bendi ya The Ngoma Africa aka FFU yenye makao ujerumani,
Ras makunja anajulikana kwa tungo za nyimbo zake ambazo mara nyingi zimekuwa zinagusia maswala ya
jamii yakiwemo "Rushwa",Ulevi,mateso ya watoto n.k pia nyimbo zake kama vile "Apache wacha Pombe",
"Rushwa ni hadui wa haki" "Wivu ni Kidonda" n.k ambazo zinafanya vema katika vituo vya redio vya ndani na
nje ya nchi pia zinapatikana www.myspace.com/thengomaafrica mchango wake ni mkubwa kwa jamii kuliko
wa wanamziki wa nchi jirani ambao kamati ya Kili Award itawapa tuzo.
Wanamziki wengine ambao wanafanya vema ni Ras Nas anaefanyia shughuli zake Norway,Fresh Jumbe Mkuu
anayefanyia kazi zake Japan.
Wimbi la malalamiko ya wadau na washabiki kama hayatatiliwa maanani na kamati ya Kili Award,basi kamati
itajikuta inawapa Award wanamziki mabao sio walengwa katika Kili Award,na matokeo yake ni kuwatosa watoto
wa tanzania ambao wanaitangaza tanzania kimataifa katika njia ya mziki.Kamati ya Kili Award hisipo angalia
kwa undani nini?nia na madhumuni ya Award hiyo itajikuta ikitoa award ya Kili kwa wanamziki wasio walengwa
kwa kigezo cha "huruma" wakati inaeleweka wazi kuwa penye "haki" hakuna huruma

WADAU MNASEMAJE JUU YA HOJA HII YA MSEMA KWELI...

No comments: