Tuesday, December 22, 2009

VETO YA SUGU DIAMOND JUBILEE... 24 DESEMBA


Maandalizi ya Uzinduzi wa Albamu ya Mr II ya VETO yamekamilika na kuwataja profesa j,joh makini,ngwea,fid q,jay moe kuwa watapamba uzinduzi huo.

Akiongea na blog hii kwa simu , Mr II amesema kuwa mbali ya wanamuziki hao walikwisha thibitisha ushiriki wao pia kua vikundi na watu kama Geez Mabovu,Kikosi cha Mizinga,Isanga family,Babuu wa kitaa,Dogo hamidu na wengineo wengi.

Ka ujumla kila kitu kiko poa alisema kwa kujiamini Mr II aka Sugu

Albam hiyo ambayo tayari imeshatanguliza ngoma moja mtaani inayokwenda kwa jina la Hold On, itakuwa ikiongelea maisha halisi ya mtanzania, na ni albamu ya kwanza ya mtanzania anayeishi nje ya bongo , kuongelea maisha ya kizalendo ya nyumbani.

Tarehe ya uzinduzi imeshatangazwa, kwamba itakuwa katika mkesha wa krismas, na 80%, ya walioshirikishwa katika albam watakuwepo jukwaani kuonesha nini kinakuwaje.

BIG UP SUGU WE ARE WAITING FOR THE MASSIVE SHOW!!!

No comments: