Tuesday, July 15, 2008

TUZO FEKI ZA KILI-2008 EPISODE 1


Tuzo za muziki dunia nzima ni kipimo cha kazi nzuri pamoja na kioo cha mafanikio kwa mwanamuziki yeyote.Hapa kwetu Tanzania tuzo hizi zilianzishwa na Hayati James Dandu aka Mtoto wa Dandu,kuanzishwa kwa tuzo hizi kulileta changamoto kwa wasanii wetu na kupata faraja kuwa kazi zao zinathaminiwa.Kila kitu kina mapungufu yake lakini naamini kuwa watu hujifunza kutokana na makosa siku zote,lakini kwa waandaaji wa tuzo hizi wamepoteza muelekeo na kufanya tuzo hizo kupoteza mvuto pamoja na maana husika,Tuzo zimekuwa Tunzo na kuwa za kibiashara na kuwakatisha tamaa wanamuziki wanaofanya kazi kwa moyo wote na nguzu zote.Matatizo yamezidi mafanikio, na malalamishi yamezidi,kwa mtazamo wangu naona tuzo hizi ni feki na zipo kwa manufaa ya watu wachache wanaopata faida ya pesa za wadhamini wa Tuzo hizi.Unawezaje kupanga wasanii wasioimba aina moja ya muziki wagombanie tuzo moja?Je waandaji wanatumia vigezo gani?Napata mashaka kama kamati ya tuzo hizi chini ya John Mhina na John Dillinga kama wanajua muziki ni nini na madhara ya kuwapanga wasanii wachanga na wakubwa kugombea tuzo moja eti ?Nilipata mshituko niliposikia eti wameweka Kaswida katika Tuzo za Muziki wa Tanzania mwaka jana? Na baadae baada ta Bakwata kupiga makelele wakatoa kaswida katika tuzo…kumbe makelele husaidia mabadiliko sawa jamani mi navaa jukumu hili ili kuokoa muziki wetu ninaoupenda sana na unaowapa faraja watanzania wengi…ni aibu kufanya kitu bila kupata ushauri kwani kamati haina watu makini wa kufikiri hasa Tuzo zetu zinataka nini na hazitaki nini?.Kwa kuendelea hivi tuzo hizi zinapoteza muelekeo wa muziki wa Tanzania na kuwapa majonzi wasanii wetu…Kwa mpenda muziki kusikia madudu ya Tuzo hizi sio ajabu kwani wengi wemeshapaza sauti na kulaumu Tuzo hizi wakiwamo wasanii wakubwa kama Mr 2 Sugu,Jay Mo,Joh Makini,Fid Q hata swahiba wangu Chief Rumanyika aka Soggy kusikika ila waandaaji hujifanya hawasikii na kuendelea kufanya mambo ya kitoto kama vile hizo ni tuzo za familia zao…inaniuma sana kuona eti waandaaji wanampa eti Tuzo Bushoke kwa wimbo ambao sio wa Bushoke ni Mwanamuziki Juliana Kanyomozi wa Uganda,na kumnyima Tuzo Tid aka Khalid Mohamed na wimbo wake wa Nyota yako! Kingine cha kusikitisha ni kuwa wimbo huo ambao Bushike ameshindia sio tu kuwa sio wake bali si wimbo wa mwaka jana kama tuzo zenyewe zinavyotaka!Ni aibu kubwa hata mwenyewe Juliana akiwa Uganda akisikia atasikitika sana na ambacho kimetokea….Unawezaje kujua albamu hii ni bora bila kujua imeweza kuuza nakala ngapi sokoni?Unawezaje kumuweka mwanamuziki mwenye albamu moja kugombania tuzo ya mtunzi bora wa muziki?sioni maana ya kumuweka msanii mwenye albamu moja, eti mwaka jana walimuweka Ally choki agombanie Tuzo ya mtunzi bora na mtunzi kama Hayati TX Moshi William?Huwezi kupata washindi wa tuzo kwa kupigiwa kura na wananchi eti kwa meseji za simu nani ana uhakika kwamba wote wanaoshinda huwa wanapata kura nyingi za sms?nani ana uhakika hizo sms zinahesabiwa kwa umakini na bila mapenzi binafsi za waandaaji?ni lini titapata washindi wa kweli katika Tuzo zetu za Kilimanjaro ?Ni wakati wa wanamuziki wa Tanzania kuamini kuwa Tuzo hizo ni feki na hazina maana katika muziki wetu.Kwani waandaji hawaoni mfumo unaotumika kupata washindi kwenye Kora au hata Tuzo kubwa duniani kama Grammy za marekani?Sasa basi nasema inatosha kupata kero za Kili kila mwaka,nilitumaini baada ya marehemu James Dandu kufariki na Kilimanjaro kuamua kuendeleza aliofanya James Dandu niliamini mambo yatakuwa bora mwaka hadi mwaka nasikitika kuona mambo yanakuwa ovyo na uchafu unaoendelea ni mwingi unaoharibu muziki wetu…Basata wapo?nashangaa miaka yote mambo yanatokea ila wao hukaa kimya na bila kuchukua hatua yoyote…au wakishapata mgao wao wa pesa toka TBL basi huwa mabubu?Pole sana Tid na yaliokipata wewe sio wa kwanza kupata aibu na kudhalilishwa na Tuzo ambazo mimi na wapenda sanaa Tanzania tuliamini zitakuwa zinawapa motisha wasanii wetu na kuenzi kazi zao wanazofanya kwa umakini mkubwa na inauma sana kuona watu wanaopanga Tuzo ili kuwasononesha wanamuziki wazuri na kuwapa wasanii wao wanaopata manufaa kupitia migongo yao…John Mhina na kamati yako maandalizi sasa ni wakati wa kuwaaachia na wengine ambao ni makini kufanya jukumu hilo na kuandaa hizo Tuzo maana naona uwezo wenu wa kufikiri umefikia kikomo...Ni aibu kwa kampuni kubwa kama ya TBL kuendelea kudhamini Tuzo zilizopoteza muelekeo kama za Kilimanjaro Music Awards na kuharibu sura ya kibiashara ya Bia ya Kilimanjaro.


Pamoja sana…..comments or call me 255 715 000 890Editor Edwin mac Temba

No comments: