Tuesday, April 01, 2008

TOKA NIGGER JAY MPAKA PROF JAY ALUTA CONTINUA!!!


Ni MC Shupavu, Joseph Haule a.k.a Prof Jay,tayari amekwishakamilisha albam lake jipya alilolipa jina la ‘Aluta Continua’, ambalo linatarajiwa kuwekwa hadharani Aprili 4, ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Akiongea na mwandishi wa blog hii kali ...Jay alisema kuwa hivi sasa atapotea kidogo kidogo mtaani...kwani yuko kwenye maandalizi mazito kama Bruce Lee kwa ajili ya uzinduzi huo.


Jay ambaye kwasasa anatamba na songi lake jipya liitwalo 'Nang'atuka,alisema kuwa albamu hiyo itabeba jumla ya track 10 za kutisha....kwani yeye ni mmoja wasanii adimu wenye kujua nini hasa wapenzi na mashabiki wake wanachohitaji kwa wakati huo.

Katika uzinduzi huo wa nguli wa muziki wa Hip hop hapa Tanzania Profesa Jay atasindikizwa na wasanii mbalimbali mahiri wakiwamo kutoka nchini Uganda, Kenya na hapa Bongo na kuwataja kuwa ni Jose Chameleon na Blue 3 kutoka Uganda huku kutoka Kenya ni Jua Kali wakati wa Tanzania, ni Ambwene Yessayah ‘AY’, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’, Besta na Rehema Chalamila ‘Ray C’.

Wengine ni Feruzi Mrisho ‘Ferooz’, Issa Shaaban ‘Matonya’, Lawrence Malima ‘Marlow’, Mandojo na Domo Kaya pamoja na Nako 2 Nako Soldiers na wengineo wengi.

Baada ya uzinduzi huo...kitakachofuata ni kupeleka burudani hiyo katika mikoa mingine minane...ambayo ni Mbeya, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro na Mara.

Uzinduzi huu unaletwa kwenu na SM, kwa ushirikiano na kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na EATV pamoja East Africa Radio.

Haya masela kaeni mkao wa kula kwani Jay anasema ana deni kubwa kwa mashabiki wake wa Dar na kuahidi kumaliza deni hilo Aprili 4.
BIG UP NIGGA JAY AKA J-O-S-E-P-H AKA PROF JAY I BELIEVE ALUTA CONTINUA!!!

No comments: