Saturday, February 23, 2008

RE:MJOMBA KADUGUDA AKIWA BWAKSI!!!


Dear Sports fans!!!

Ni aibu sana kwa kiongozi kama huyu wa simba kuutwika mtungi na kusinzia katika hafla muhimu kama hii iliyoandaliwa na TASWA Diamond Jubilee jana kuwapa Tuzo wanamichezo bora wa mwaka-2007.Je swali linakuja?Kaduguda hana pesa ya kunywa mpaka kwenda kufakamia pombe za bure kwenye party ya Taswa?ni aibu kubwa kwa Katibu wa timu kubwa kama Simba SC kuwa katika hali hii katika sherehe za kuzawadia wanamichezo.Nafikiri mtu kama Kaduguda anapaswa kuwa makini na hafla kama hizi maana yeye ni Kiongozi wa mpira na kiongozi wa timu kubwa kama Simba SC,haya ni mambo ambayo kwa njia moja au nyingine yanadidimiza soka la nchi yetu.Je wanachama wa Simba SC wanamchukuliaje Katibu wao???au wao wanaona ni vizuri...mmmh sijui labda Kaduguda ndio mhimili wa soka la Simba Sc...Ni hayo tuu wananchi na wapenda soka kuamka na kuachana na viongozi wa namna hii ya Kaduguda.

Ni hayo tu kwa leo na mtazamo wangu huu.


Mac Temba Jr.

No comments: