Tuesday, December 18, 2007

OKOA HIP HOP PROJECT

OKOA HIP HOP BONGO!









Kilio cha mashabiki wa hip hop kuhusiana na kudidimia kwa muziki huo safari hii kimeonekana kupata utatuzi baada ya baadhi ya wakali wa muziki wa hip hop nchini kuamua kujitoa muhanga na kuiokoa kwa kufanya kitu ambacho kinatarajiwa kuwa ni mapinduzi ya aina yake, kitakachopelekea muziki huo kurudi kwenye ramani kama ilivyokuwa long time.

Okoa Hip hop ni mradi maalum uliobuniwa na msanii Adili a.k.a Hisabati ambaye amekuwa akipigana vilivyo kuhakikisha muziki huo unasimama na kufanya vizuri kama ilivyo aina nyingine za miziki hapa nchini “unajua Hip Hop haina special package kama ilivyo aina nyingine ya miziki kwani wadau wenyewe wametoa macho kwenye bongo fl eva ambayo hivi sasa imekuwa ikithaminiwa wakati ni muziki unaoongoza kwa kuipotosha jamii” alisema Adili ambaye ndiye kiongozi mbunifu katika mradi huo.

Sababu za mradi huo kuitwa Okoa ni ili ieleweke kirahisi maana hip hop inahitaji kuokolewa kabla haijapotea kabisa kwa inaaminika kuna tume maalum ambayo imekaa makini sana kuhakikisha hip hop ya kibongo haifanyi vizuri kabisa “iwapo hatutakuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunafanya hizi harakati kweli hip hop itapotea na kutakuwa hakuna wa kuikoa kwani sisi wanahip hop ndio wa kuiokoa no one else”-Adili.

Mradi unawahusha wakali wa hip hop akiwemo Jay Moe, Adili, Joh Makini, Mansu-Li, Mapacha, Blac, Salu-Te, Saigon, Magazijuto, Nako 2 Nako, Geez Mabovu hii ndio timu ya ukombozi wa hip hop na ukitazama majina haya unaweza kugundua ni aina gani ya vichwa vimeamua kuipigania hip hop. “tatizo ambalo linapelekea muziki huu kutopewa kipaumbele ni kwa kuwa wanahip hop wana akili hivyo si rahisi kuwapeleka peleka kibiashara kama ambavyo wanapelekwa wasanii wa bongo fleva hapo ndo noma inapoanziaga, kwani mameneja wengi hupenda kupiga michongo na wasanii wasio na akili na hii ni kwa ajili ya maslahi yao binafsi” alisema adili.

Ujio wa Okoa Hip hop ni wa tofauti kabisa kwani mpaka sasa wanachokifanya ni kufanya maandalizi ya mini documentary yao ambayo itakuwa ikielezea historia ya Hip hop ya bongo pamoja na kuwepo kwa video xclusive za wasanii ambao wamo katika mradi huo, mpaka sasa wasanii wote wamesharekodi ngoma zao mpya maalum kwa ajili ya kuiokoa Hip hop pamoja na video.

Documentary hiyo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni itaanzia mkoani mbeya tarehe 30, kisha kufuatia bongo ambapo shughuli zote zitakazofanyika katika ziara yao hiyo kuanzia show na kila kitu zinatarajiwa kuonekana katika documentary dvd hiyo ambapo kutaandaliwa show maalum ambayo itajulikana kwa jina la Live dvd Show itakayohusisha live showz za wasanii hao.

“Ni ngumu sana kuwakusanya wasanii wenye uwezo na kufanya nao kazi lakini mimi nimeweza kwa kuwa wote hawa nimekuwa nikifanya nao kazi tangu enzi hizo hatuna kitu mpaka leo hii walau tuna vijisenti, hii ni true lov kwa wanangu, kwani wananijua nilivyo then na mi najua walivyo bado tuko pamoja katika kutafuta na kuhakikisha malengo yanatimia, si kama najisifi a tu mzee ila jamaa wote hawa nimeishi nao vizuri sana hivyo imeniwia rahisi kuwakutanisha na kupiga nao kazi”-Adili Hisabati. Katika vitu ambavyo Adili ametaka ieleweke ni kuwa “Hip hop jamani ni Hip hop na wala haifanani na aina yoyote ya muziki nikiwa na maana ni kama soka haifungamani na upande wowote na ina sheria zake ambazo hazibadiliki, na bongo fleva haiwezi kufananishwa na hip hop hata kwa nukta, sasa kazi ya Okoa Hip hop ni kuleta mapinduzi ili ibainike kuwa Hip hop ibaki kuwa Hip hop na Bongo fl eva ibaki kuwa Bongo fleva.

Malengo yao ni kuhakikisha kila msanii anapata nafasi ya kupromote kazi zake kwani kama utakuwepo katika maonesho ya okoa utaweza kujipatia bidhaa za wasanii wa hip hop waliomo katika mradi huo iwe ni Tshirt, tape, cd na kila kitu, pia itasaidia kupush albam ambazo hazikufanya fresh sokoni itakuwa rahisi washabiki wakiibuka na kujipatia wanachotaka kiurahisi. Mwisho kabisa wanahip hop hawa wanatarajia kutengeneza fi lamu ambayo itakuwa ni ya kihip hop ile mbaya, itakayokuwa ikielezea maisha ya kisanii na hip hop ya kibongo kwa ujumla, “huu ni mwanzo tu ila tamasha la Okoa Hip hop litakuwa likifanyika kila mwaka kama yalivyo matamasha mengine” alimaliza Adili.

1 comment:

Anonymous said...

Whats up guys?
I like the idea of OKOA HIPHOP PROJECT because for real it will help the HIPHOP music industry in Tanzania. I have a question to the founders and the fans of HIPHOP in Tanzania,my reference to this project on the first time I saw the plan it was to involve various artist including Kikosi cha Mizinga but after the starting of the project I found out the guys are not included, is it because of the on going beef between Kikosi and Naco2Naco?or is it because its involvement wont bring benefits to the founders?