Tuesday, December 18, 2007

MADEE ACHA KUPOTOSHA WANA HIP HOP!!!!



Ni kichekesho na utani mkubwa kwa msanii kama Madee wa Tip Top Connections kuutangazia umma eti hip hop hailipi na yeye pia ni msanii wa hip hop na sababu hiyo anataka kubadili mfumo wa muziki wake ili aweze kuuza kama Ali Kiba,ni "kichekesho" kikubwa kama alivyoimba Witness aka coca- cola popstar katika video yake mpya....Tangu lini Madee kawa mwana Hip Hop hapa kwetu Bongo?Nikiwa mdau wa muziki huu namfahamu Madee vizuri sana tangu akiwa Underground na ndio sababu inayonifanya mimi kuandika mtazamo wangu huu,Je madee anaweza kujiita mwana hip hop kati ya wana hip hop baadhi kama Sugu aka Mr II aka HU Jintao,Kwanza Unit,Weusi Wagumu Asilia(WWA) ,Nigger J aka Prof Jizze,Imam Abass,Jay Mo,Mc Chivaro(Evalasting King of Ilala),Solo Thang,Hashim Dogo na wengine wengi walioleta mapinduzi makubwa ya muziki huu toka miaka ya tisini na tano na kuendelea...iweje Madee ajiite anaimba hip hop gani????Hip hop dunia nzima ni muziki usiokuwa na mauzo makubwa lakini ni muziki unaosaidia kuleta mabadiliko makubwa ya jamii na kukumbusha viongozi majukumu ya msingi katika kuleta mabadiliko katika jamii husika,Ni kweli kuwa Waimba Qaswida kama Ali Kiba,Mb Doggy na wengine wengi wanauza sana...Je wanaelimisha nini jamii zaidi ya kuzungumzia kitu kimoja album nzima!Je Madee angependa jamii ipate nyimbo za kitoto za kujisifia kuwa upo na msichana mrembo kama malaika wakati katika hali halisi hujapata kumuona malaika mwenyewe?Hip Hop ni muziki sahihi na unapaswa kuwepo ili jamii iweze kupata mitazamo ya ukweli na sio mambo ya kufikirika na ya ndoto,Swali jepesi la kumuuliza Madee tangu aanze kuimba amewahi kuimba wimbo gani wa Hip hop?Naamini Madee ameishiwa na anataka kutumia wimbo huo ili kupata umaarufu na kuongeza mauzo ambayo mimi naamini haitawezekana,Hip Hop ni wito ndio maana wasanii wengi wa Hip Hop hawana papara ya soko maana soko limevamiwa na waimba Qaswida,Hip Hop haitakufa maana ni muziki unaozungumzia maisha halisi na mitazamo chanya katika jamii tunayoishi,So kama madee anataka kuimba Qaswida ili aweze kuuza kama Ali Kiba ni Bora kuliko kupotosha wapenzi wa Hip hop kuwa kuliko kuimba Hip Hop ni bora kuuza pipi!Msanii anayedharau hip hop kwa mtazamo wangu ni mtu asiyejua anatoka wapi na anaelekea wapi....Ni wakati wa wasanii kufanya sanaa ya ukweli maana wale wote feki kama Madee hawana muda mrefu katika sanaa na watapotea soon

Hip Hop will not die as Nas Escobar said in his new Track....Aluta Continua
HIP HOP ALIVE!!!!

2 comments:

Anonymous said...

Kaka nimekupata! lakini mi nadhani labda turudi kwanza kwenye dhana nzima ya HIPHOP! mziki huu bila shaka ni mziki uliotumiwa kwenye movement nzima ya freedom kule marekani kwa black ethinic. hapa kwetu hiphop tumeipokea tu kama zilivyo genre nyingine za muziki(such as pop,RnB,chacha,Funky etc)...Sasa pengine niseme kuwa hata sisi tunaojifanya tunaujua huu muziki wengi wetu hatuujui bali tunakurupuka...na mara nyingi wana hiphop wengi wana inferiority complex...wao ni rahisi kuponda genre nyingine ila ukiwagusa wao basi taabu sana. kwa upana mkubwa, mziki sasa hivi ni biashara, no doubt....hata kama unafanya music for yor people they got to support financial na sidhani kama kuna mtu hapa duniani anaefanya kazi za charity..maana hata makanisani ni charity lkn wakati huo huo msako wa not. Sitaki kuamini kuwa wana hiphop wana uchungu sana na maisha ya wenzao kupita ya kwao wenyewe. Nikirudi kwa Madee, mi nadhani anaweza kujiita mwanahiphop unles mtu ajitokeze na kuniambia misingi ya hiphop inayomtofautisha madee na Mr II, mwanafa na chidi benzino, AY na Adili. mi nadhani hiphop sio Biti (eti hii ni bongo flava na hii ni hiphop)...la hasha, hiphop ni zile nguzo tano ambazo nikiziangalia kwa umakini,sioni mmbongo yoyote yule anaweza kujiita mwana hiphop...wote tunaganga njaa kwa kutumia njia nyingi ikiwepo hii ya woga wa wanaojiita wana hiphop ku seek sympath za mashabiki. kukubwa hapa ni kuwa rela, most of the so called bongo-hiphop artist hawana hata knowledge ya Tanzania, matatizo yanaowakumba watanzania,mazuri ya Tazania etc. na hata wanaojua basi watabahatisha kwenye mistari miwili mitatu isiyo na connection ili mradi vina vipo na katika topic zao wamedisi bongoflava..na kukunja sura zao tu ili waonekane wagumu..hakuna la msingi..ni wachache sana angalau wanaweza kusema wamefikisha ujumbe kwa adhira kwa zaidi ya nyimbo 10 zenye maana..wengi wao watatoka na nyimbo moja kali hlf ningine wack mpaka wanaingia kaburini..lets be honest, mimi nakubali adili kazi anayofanya ya video production..lkn as an artist, what is his contribution kwenye hiphop.....Peke Yangu? contribution ya hao mapacha ipo wapi katika jamii, huyo superstaa wa cocacola kashafanya nini cha ajabu kwenye hiphop? au tuseme hao jamaa wa kikosi wanaopiga kelele kila siku..wamefanya nini zaidi ya fujo? hebu jaribu kulinganisha tungo zao na madee wanaomponda..unapata picha gani? Mimi nawakubali sana watu kama Proff J,mwamba wa kaskazini,chid benzino,MwanaFA na wengine wachache..angalia mashairi yao..no beef, mashari yana ujumbe ulionyooka na yana connection na jamii..wengine waliobaki....hata Mr. II nawaona ni wack..no disrespect kwa mr. II, amefanya kazi nzuri ya kusaidia mziki wa kizazi kipya kukua(si hiphop, naomba nieleweke)..nadhani madee alitoa mawazo yake binafsiyanayolenga ukweli..mimi nadhani wanaojiita wana hiphop wachukulie hiyo kama challenge..na sio kupiga makelele yasio na msingi.

Anonymous said...

naongezea tu kwa kusema kuwa, OKOA HIPHOP sio kuvaa T-shirt zilizoandikwa ujumbe huo..bali ni ku arrange matamasha ya kutafuta vipaji kama lile linaloendeshwa na channel-O. nashukuru kwamba Adili alishiriki japo aibu ilimkuta(siku diss) lkn msingi mmojawapo wa hiphop(freestyle) ulidhihirika kuwa kwa hapa bongo wana hiphop wengi ni wachovu..big up kwa imam abbas na mwakilishi wetu wa Tanzania, that is what we call Nanihii!. I'am very hiphop fan na nimezunguka kwa miguu kutoka bongoyo road mpaka masaki kwenda kurekodi hiphop kwenye tapes(chrome) kutoka kwa washkaji waliokuwa wanarudi likizo kutoka mamtoni enzi hizo..lkn lazima nikubali mabadiliko ya muziki..usipokubaliana na maadiliko then wewe ni MWOGA..kasome kitabu cha 5th Discipline cha PETE SENGE kuhusu mabadiliko. ni kuwa enzi zetu za kusikia boom bap za producers like peterock,Dj premier,Large proffessor, Malleymal, zimeshapita na lazima tukubali..sio kwamba wao jamaa hawapo tight anymore..la hasha bali ni kuwa zama za hiphop ya wakati wao imeshachange sana...bado ni wakali lkn ukitaka kujua zama basi agalia dr. dre na Htech...bado wana survive kwa kuwa wanajua mabadiliko...mpaka leo they are regarded as producer officianados..lkn hebu angalia beat ya sasa ya Dre na zile za deathrow... zimechange sana..ila msela haja loose identity yake...nimetoa huo mfano ili watu tujiangalie na tukubali mabadiliko,tukubali kukosolewa na tuangalie wapi pa kuanzia ili kuendeza dhana nzima ya hiphopna benefits zake..lkn sio kwenda kwenye interview, kulaumu wahindi(of course ni wanyonyaji..lkn hawanyonyi hiphop peke yake) na radio stations.....tubadilike hasa katika knowledge..we are lac of knowledge that why aour lyrics are wack and even our thot is wack. vueni hizo Tshirts zenu na muingie mtaani ku support vipaji..na sio kuganga njaa kama kweli mna moyo wa kuendeleza hiphop..ni mawazo yangu tu kama yalivyo ya madee, na MACTEMBA(my borther)