Thursday, May 06, 2010

KALAPINA AJITOSA UDIWANI KINONDONI KUPITIA CUF

MSANII mahiri wa muziki wa Hip Hop Tanzania, Kalama Masoud ‘Kalapina’ ametangaza kujitosa kuwania udiwani katika mojawapo ya kata zilizopo wilayani Kinondoni katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kalapina ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Kikosi cha Mizinga la Kinondoni jijini Dar es Salaam, alisema kuwa, anapenda sana siasa na ipo kwenye damu yake, ndiyo maana nyimbo zake nyingi amezielekeza kwa jamii.
Aidha Kalapina maarufu kwa jina la ‘Pina’ alisema kuwa, lengo lake jingine la kuwania nafasi hiyo ni kuwasaidia wakazi wa kata hiyo atakayogombea, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiongozwa na viongozi wanaojinufaisha wenyewe pasipo kuangalia maslahi ya wapiga kura wao.
“Unajua ni muda mrefu viongozi wanaoiongoza kata ile wamekuwa na propoganda zisizokuwa maana yoyote, matokeo yake wananchi wamekuwa wakiteseka kila siku, sasa lengo langu ni kuleta mapindizi ya kweli katika kata ile,” alisema Pina ambaye hakuwa tayari kuitaja kata hiyo atakayowania.


Kalapina anagombea kiti cha udiwani kata ya kinondoni mjini kwa kupitia tiketi ya chama cha wananchi CUF.
HONGERA SANA MWANAHARAKATI KALA PINA.

No comments: