Sunday, November 29, 2009

MAXIMO INATOSHA....TUMECHOKA!!!
Ndugu zangu wadau mi naomba kuwauliza na nyie hivi huyu maximo ananganganiwa kwanini na TFF na serikali wakati anabolonga sana na kutufanya sisi kama wajinga na wasiojua nini maana ya mafanikio katika soka,hivi huyu maximo ana mpango gani na timu yetu???Huyu tuliyedhani ni mkombozi wetu eti kaanza kua act movie na wakina kanumba na kuacha ku focus na kua analyze maendeleo ya soka letu...nahisi huyu mtu kapoteza mwelekeo na anapaswa kuondoka na kutuachia timu yetu...ni aibu kubwa kumpanga kipa Muharami eti kisa maximo kaambiwa huko Msumbiji anadaka sana hivi kweli huyu maximo anataka kudhibitisha nini kwetu huyu mwarami tunamjua tangu mwanzo ni mwehu na sio makini awapo golini na hana jipya hivi maximo na chuki zake kwa kaseja ndio zitugharimu mamilioni ya watanzania wanaopenda soka??Hivi hata hao wadhamini wanachukuliaje hali hii ya timu yetu?????Nani anabisha kuwa Kaseja ndie kipa bora hapa Tanzania???Kwani maximo kashawahi kukosewa mara ngapi na wachezaji tangu aanze kufundisha soka???ndio hata huko alikotoka ndio staili yake hii???Rooney ni mfano wa mchezaji ambaye alikuwa na utovu mkubwa wa nidhamu lakini alilindwa na kusaidiuwa ili kubadilika na ona sasa alivyo ni msaada tosha kwa timu ya taifa na klabu pia...huyu maximo halioni hili????Mbona Leodgar Tenga anapoteza muelekeo???Mafanikio ya kocha dunia nzima ni kushinda sasa huyu maximoana msaada gani kwetu????Eti kwani zanzibar wana kocha mzungu???mbona wanacheza soka zuri na kutoa dozi la maana!!!!!Hivi maximo anakumbuka jinsi alivyokaribishwa alivyoingia hapa tanzania???hivi anajua watanzania hawapendi masihara na ujinga???hivi anajua pesa anayolipwa ni hela ya walipa kodi wa tanzania???tangu kaja tumeshindwa kupata hata kombe moja???Jose mourihno na alex furgeson wanasifika kuwa makocha bora sio kwa sifa zao bali kwa kusaidia timu zao kupata mataji huyu maximo anasaidia nini kwetu???Inatia kichefuchefu kuona timu ya taifa inayotunzwa kama wafalme wakiwa kambini,jezi na malazi ya kisasa bado inasuasua katika mashindano.
ki ukweli maximo amechoka na hana jipya tumechoaka na tumechoka sana,ni muda wa kufanya mabadiliko makubwa kwenye timu yetu na benchi la ufundi ili tuweze kupata mafanikio tunayoyataka.Hivi Kaseja kamfanya nini maximo jamani?????au kuna lingine ambalo halizungumziki????Sawa maximo hapaswi kuingiliwa kwenye maamuzi yake but Tenga na Mwakalebela amkeni na muisaidie Taifa stars iweze kupata muelekeo sahihi.
Jamani tusimame na kumwambia maximo inatosha na aende kwao atuachie timu yetu maana anaipaka shombo na hana msaada,let him join kanumba kwenye movie naona ndio amepanga kumalizia career yake.
Inakera sana kocha anayepewa mamilioni ya hela za walipa kodi halafu anashindwa kutupa burudani,na kutufanya sisi kama mazezeta tusiojua soka,kila siku anaita timu mpya ya taifa na visingizio vingi mara huyu ana hili mara vile ili mradi tu aongee na vyombo vya habari.
Nakumbuka Maneno ya Kocha mkongwe Mziray aliyesema hata yeye angepewa timu ya taifa kipindi hiki ambacho serikali inaisaidia na kuwapa msaada wa kila hali angefanya makubwa katika soka letu,ni kweli kabisa sio kwamba makocha wetu walishindwa kuleta changamoto taifa stars ila kipindi cha nyuma serikali iliisusa timu ya taifa,timu ilikuwa inakaa kambini salvation army na kula chakula hafifu lakini waliweza kuchukua kombe la chalenji na kuipa nchi sifa kubwa.
Maximo amekosa jipya kwetu,dunia nzima timu ya taifa haibadilishwi kama nguo,asubuhi blue,mchana kijani mara jioni nyeusi hi staili ya wapi????timu ile iliyowafunga Burkina faso ilikuwa na udhaifu gani mpaka hakuendelea nayo???Mimi sina chuki na maximo bali kwa mtazamo ulio wazi kuwa maximo na uwezo wake umefikia mwisho na safari yake imewadia.
Leodgar Tenga amka na uwaonyeshe watanzania kuwa wewe ni kiongozi makini na wala sio kibaraka uliwekwa hapo kwa masilahi ya watu Fulani.
Kesho twacheza na Zanzibar,ambao jana waliwafunga Burundi goli 4 za ukweli,kama kawaida zenji watatufunga na kurudi hapa kupiga domo ooh mara hivi mara vile wallahi huyu maximo angekuwa enzi za mwalimu angemtimua kwa bakora ili akamuonyeshe mkewe.
Je Kenya wana kocha mzungu???Uganda wana kocha mzungu???Zanzibar nao wanae??????

TUMECHOKA MAXIMO TUMECHOKA NA STAILI YAKO……NENDA MAXIMO

ni mimi mdau mwenye majonzi

MAC TEMBA JR

No comments: