Wednesday, October 21, 2009

HUU NI UNYAMA SANA KWA MTOTO HUYU
KAMA ULISIKILIZA VIZURI LEO TENA NA DINA MARIOUS CLOUDS FM KIPENGELE CHA HEKAHEKA NA GEA HABIB, HUYU NDIYE MTOTO SIMULA MAGATHI (MIEZI 5) WA MKOANI MARA ALIYEKATWA VIGANJA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA NA MTU ASIYEJULIKANA KISA VINA MICHORO YA MIKUNJO HERUFI M. AKISIMULIA TUKIO HILI BIBI WA MTOTO HUYU NYAPAMBA MAGATHI AMESEMA ILIKUWA NI KTK SHUGHULI ZA MAISHA AMBAPO ALIMWACHA AKIWA AMELALA HUKU MTOTO MWINGINE MKUBWA AKICHUNGA NYUMBA ALIPOREJEA AKAKUTA CHUMBA KIMEJAA DAMU NAKUJIONEA KILICHOTOKEA ASIJUE KIMETENDEKA VIPI, ALIYE FANYA UNYAMA HUU MPAKA SASA HAJAPATIKANA NA HAKUNA JUHUDI ZOZOTE ZINAZOFANYWA NAJESHI LA POLISI KUPELELEZA HATIMAYE MBAYA KUBAINIKA. "INATISHA INAHUZUNISHA" MTOTO SIMULA MAGATHI ANAISHI NA BIBI YAKE KWANI MAMA MZAZI WA MTOTO HUYU NYASATO SIMULA NI MGONJWA WA AKILI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MKOA WA MARA. PICHANI MTOTO SIMULA MAGATHI AKIWA USINGIZINI NDANI YA HOSPITALI KUU YA MKOA WA MARA AMBAPO ANAPATA MATIBABU. UNYAMAGANI HUU.

JAMII TUKEMEE UONEVU HUU.....JAMANI INASIKITISHA SANA!!!!

No comments: