Friday, September 18, 2009

VODACOM BUSINESS YAFUTURISHA WATOTO YATIMA WA CHAKUWAMA –SINZA MORIKatika utaratibu wake wa kila mara kampuni ya simu za mikononi Vodacom Tanzania kupitia kitengo chake cha Vodacom Business jana ilifuturisha watoto katika kituo cha kulelea watoto yatima CHAKUWAMA kilichopo Sinza Mori jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya futari hiyo mratibu wa shughuli za kituo hicho kutoka Vodacom Edwin Temba aliwataka watoto hao kujiamini katika mambo yao mbalimbali wanayoyafanya kwani kujiamini kwao kutawafanya kushinda matatizo yoyote yatakayowakabili, Edwin aliongeza kwamba wao ni sawa na watoto wengine, kwani wanaweza kuwa wa kwanza kimasomo shuleni lakini pia wanaweza kuwa wa mwisho kimasomo hivyo kufanya vizuri kwao kutategemea jitihada zao katika masomo.
Naye mfanyakzai mwingine kutoka Vodacom Esther Mattle aliwaambia watoto hao kuwa Rais wa nchi hii Mh. Jakaya Kikwete alikuwa mtoto kama wao, lakini alikuwa msikivu kwa wazazi wake na watu wazima ndiyo maana akafikia mafanikio hata kuwa rais wa nchi hii, hivyo akawataka watoto hao kuzingatia yale yote wanayomabiwa na watu wazima pamoja na walezi wao, Vodacom pia walikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto hao ikiwa ni pamoja na unga, mafuta ya kupikia, sabuni na vifaa vya kuchezea watoto.

1 comment:

Anonymous said...

ndugu yangu vodacodacom m mko juu mdau wa blog hii uko voda nini ?

hongereni vo