Wednesday, April 15, 2009

VODACOM MARATHON...FOMU ZATOKA LEO


Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nector Pendaeli Foya (kushoto) akionyesha mfano wa fomu zitakazotumika kuwaandikisha washiriki wa mbio za riadha zijulikanazo kama Vodacom Dar Marathon katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Fomu hizo zitapatikana kwenye maduka ya Vodashop sehemu mbalimbali nchini. Mbio zinatarajiwa kufanyika Juni 21 jijini humo. Kulia ni Ofisa Habari wa kampuni hiyo, Matina Nkurlu

Kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania imewataka washiriki wa mashindano ya riadha maarufu kama Vodacom Dar es Salaam marathon kuanza kuchukua fomu za ushirki katika maduka yake ya Vodashop.
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi, Nector Foya alisema Jijini jana kwamba mbali na Vodashop za Dar es Salaam pia fomu hizo zinapatikana katika Vodashop zilizoko katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.Alisema mshindi wa kwanza kwa Kilomita 21 atajinyakulia shilingi milioni moja(1000,000) ,mshindi wa pili atanyakua Shilingi laki sita( 600,000, )Mshindi wa Tatu atazawadiwa Shilingi laki nne na nusu( 450,000) na wa nne Shilingi 300,000.
Alisema mshindi wa tano Shilingi 150,000 wakati wa sita hadi wa 10 watajishindia Shilingi 50,000.
“Hivyo nachukua nafasi hii kuwaomba watu kujitokeza kwa wingi ili kujishindia zawadi mbalimbali pamoja na kuonyesha vipaji vyao,”Kwa upande wa mbio za kujifurahisha alisema washindi watazawadiwa zawadi za papo kwa papo, washiriki wa mbio hizi ni wale wenye umri wa kuanzia miaka 10 na kuendelea wakati wale wa mbio za kilomita 21 ni wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Alifafanua kwamba lengo la mashindano haya ni kukuza mchezo wa riadha hapa nchini kwani mbali na kuwa ni mchezo unaopendwa na watu wengi pia ni mchezo ambao kwa miaka mingi umekuwa ikililetea heshima taifa letu .Alisema riadha imekuwa ni mkombozi kwani pale inapotokea kwamba michezo mingine haifanyi vizuri, riadha ndiyo pekee umekuwa mkombozi wetu, tunaona fahari kushiriki katika kuwekeza katika mchezo huu.
Mbali na raidha, pia Vodacom Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza michezo hapa nchini, baadhi ya michezo ambayo Vodacom imekuwa ikiwekeza ni pamoja na Mpira wa Miguu, mashindano ya Basikeli, mashindano ya Vodacom Miss Tanzania, kombe la Muungano.
Michezo mingine ni pamoja na mashindano kuogelea, tenesi, Golf na hivi sasa shindano la kuwasaka vijana wenye vipaji kote nchini maarufu kama la Bongo Star Search(BSS)
BIG UP VODACOM...PAMOJA DAIMA

No comments: