Monday, August 18, 2008

YAKO WAPI MAPINDUZI YA HIP HOP- BONGO

Neno mapinduzi ni neno linalobeba maana kubwa sana yaani mabadiliko makubwa ya kutoka aina Fulani ya maisha na kwenda mfumo mwingine wa maisha,au kutoka aina Fulani ya mtazamo na kwenda kwenye mtazamo mwingine tofauti…Muziki wetu wa Hip Hop kwa muda mrefu umekuwa ukikubwa na mambo mengi ambayo huchangia kurudisha nyuma juhudi za wasanii wa muziki huu kujikwamua na kuweza kufikia malengo yao kisanaa,kufikia malengo ni kumaanisha kama kuweza kuuza nakala nyingi za albamu zao ili kuweza kujikimu kimaisha na kuweza kupata faida kwenye muziki wanaoufanya…Huwezi kufurahia muziki ambao haukusaidii kimaisha! Soko la muziki huu limekuwa gumzo lisilokwisha kwa wasanii wa muziki huu…Wasambazaji wa kazi za wasanii hapa bongo kama Mamu stores na Wananchi stores aka Wadosi wanalaumiwa kwa kuwabana sana wasanii wa Hip Hop tofauti na wasanii wa Bongo flava,si jambo la kiungwana kwa msambazaji kumpangia mnunuzi aina ya bidhaa inayotakiwa kuingia sokoni…msambazaji anapaswa kupokea kazi zote na kuzifanyia matangazo ili mnunuzi apate bidhaa tofauti sokoni tofauti na hivi sasa wakati soko letu limetawaliwa na aina moja ya bidhaa sokoni!!!Je kwani Hip Hop albums sokoni ni mpaka Prof Jay atoe albamu ndio wahindi wa GMC waamue kusambaza?Mbona wasanii wa Hip Hop wapo wengi kama wakina Geez Mabovu,Mapacha,Blac na wengine wengi lakini mbona hawapati sapoti ya kweli ili na wao wakapata mafanikio kama wengine wabana pua aka Bongo flava???
Ipo wapi OKOA HIP HOP Ya Mwanamapinduzi Adili???nilipopata wasaa wa kupata ripoti ya mkakati huu miezi michache iliyopita ya mradi huu nilipata faraja nikasema sasa wana hip hop wamepata mahali na jukwaa la kusemea mambo yao ili kuifunza jamii na kuisaidia jamii yetu inayokabiliwa na matatizo mengi kama rushwa,ufisadi na mengineyo,hii ilitokana na kumwamini sana Mdau wa hip hop Adili Mkwela aka Chapakazi niliposikia amechukua jukumu hili niliamini yatawezekana pamoja na kuwa na mizengwe sana ila kwa sapoti ya wapenda hip -hop yote yangekwenda shwari…ila kwa mtazamo wangu naona mradi huo wa Okoa Hip hop umeishia magazetini na kwangu mimi ni pigo kubwa sana maana lile lengo la kuwanyanyua wasanii hawa wa Hip hop limeishia njia panda na ki ukweli haya yanayoitwa mapinduzi kila siku yanakosa maana na kuishia mapinduzi feki ya mbwembwe nyingi magazetini.Wadau wa Hip hop wapo wapi?Mpaka lini mambo haya yataendelea kufumbiwa macho ?Hivi tutaendelea kweli mpaka lini kusikiliza nyimbo za kitoto za mapenzi na ndoto mpaka lini?jamii yetu inapambana na matatizo mengi sana kipindi hiki kama wanasiasa waongo na walaghai kama alivyosema msanii wa hip hop wa kike Nakaaya Sumari kwenye wimbo wake wa “Mr Poilitician”.Mada ni nyingi za kuzungumzia ila wasiotakia heri muziki huu hufumbia macho mambo haya na kuacha wasanii wetu kuimba nyimbo za kitoto na zisizokaa sokoni zaidi ya mwezi…Nakumbuka shindano la Tusker Project fame,” jaji mmoja wa Kenya Mr Ian alisema muziki wa Tanzania wa Bongo flava ni muziki wa kutamba mwezi mmoja na kupotea”,hii ni kweli maana wimbo uiotoka mwezi wa tatu mwaka huu hata haukumbukwi tena maana nyimbo zenyewe huwa ni za mashairi ya kuzungumzia mambo ya kitoto na ndoto nyingi kama vile “nipo angani naendesha gari la milango 20 “na mambo mengine kama hayo ambayo katika hali ya kawaida huwa ni ndoto na mambo ya kufikirika ambayo hayana uhalisia hata kidogo kwa mtu makini kusiiliza zaidi ya watoto wa chekechea kwasababu kwao huwa ni vichekesho kama mtu kubeba ghorofa..
Ushauri wangu kwa wadau wote ni kuwa hakuna mapinduzi ambayo hayana mipango na mikakati(Strategic plan)..waulizeni hata maveterani wa mapinduzi ya Zanzibar ya kumtoa Sultan walitengeneza mkakati na ndio maana walifanikiwa,ni jukumu la wasanii wa Hip hop kuungana na kuwa na sauti moja ili kuweza kufikia malengo husika,hakuna mapinduzi ya mtu mmoja mmoja! Ni wakati wa kuwa na mtazamo chanya na kufungua macho kutokomeza hali hii ya kudidimiza muziki huu wa Hip Hop hapa nchini kwetu Tanzania,haya yatafanikiwa ikiwa wana hip hop watakuwa na sauti moja na kuacha unafiki kati yao na kuacha bifu zisizojenga wala kusaidia sanaa hii ili waweze kuwapa wananchi msaada wa kuzunguzia shida na matatizo yanayozikumba jamii zetu za kitanzania.
Mungu ibariki Tanzania,Mungu ubariki muziki wetu.

Ni hayo tu,kwa maoni na ushauri tembelea blogu yangu
www.mactemba.blogspot.com au email mactemba2000@yahoo.com au simu namba 0715 000 890

No comments: