Saturday, August 02, 2008

WARAKA WA PILI-KILI AWARDS-2008



Baada ya kutoa waraka wa kwanza wiki iliyopita kuhsu Tuzo za Kili za mwaka huu nimepokea simu nyingi na meseji nyingi za wananchi wakataka kupata dodoso kuhusu mambo mengi yaliojili katika Tuzo za mwaka huu ambazo mimi Mpiganaji nimeamua kuvaa mabomu kama Mpalestina au Mshia wa Iraq kukomaa na wadau wenzangu paka tupate muelekeo ambao utafanya Tuzo hizi ziwe za kiungwana na kuheshimu wapenzi wa muziki wa nchi hii kama sio Kisiwa hiki cha kusadikika mpaka kieleweke!
Katika maswali ambayo watu wengi hujiuliza ni kwamba nani wapo nyuma ya Tuzo zetu za muziki mpaka mwaka hadi mwaka tuendelee kusuasua na kuwapa Tuzo watu wasio stahili,Kwani Kamati ya Kili Awards huchaguliwa na nani???na hufanya kazi kwa manufaa ya wadau wa muziki au Wadhamini Kilimanjaro lager?Nini nafasi ya chombo kama BASATA katika Tuzo hizi???Watu wengi walionitumia sms wanagusia kwamba Tuzo hizi zimekuwa zinatumiwa na wadau Fulani kuweza kuwatoa sokoni wasanii wao ili kupata mauzo na kuweza kung’aa katika medani ya muziki wetu…kwa mfano mwaka jana Tuzo ya mwanamuziki bora wa R&B alipewa msanii Q-jay wakati huo kijana huyo alikuwa na Single moja wala hakuwa na Album sokoni wakati huo!!! Hii ni hatari sana na inaonyesha wazi kuna watu wanaoweka tuzo kwa wasanii wao kwa lazima wapate…inakuwaje eti msanii mmoja kuwa katika category ya tuzo peke yake???Hii ni danganya toto ili mradi tu kupeana Tuzo ki lazima…
Kwa wapenda kuangalia runinga watakwambia kuwa video za Visual Lab Nexl Level chini ya Adam juma zilikuwa kwenye Top ten za vituo vyote so inasikitisha kuona majaji wanaenda kinyume na mambo yalio wazi na ambayo hayahitaji kwenda sana shule!!! Nymbo za mwaka jana zilishikwa na Ambrose Dunga wa Lebo ya 41 Records mmmh lakini majaji wetu si ni wana makengeza au ni kujitoa akili wakampa produza ambae kwangu mimi naamini mwaka jana hakushika chati katika nyimbo 20 zilizoshika hapa Bongo….Hivi kwenye Kili majaji wetu wanaabudu ubaguzi ambao hata Mwanzilishi wa Taifa hili aliupiga vita…Eti Akudo na FM Akademia wakawatoa eti ni Wacongo!!! Basi ilikuwaje wakawaita kama watumbuizaji katika hafla hiyo wakati zipo bendi nyingi za asili hapa kwetu kama Tatu Nane,Paparanda Arts na nyingine nyingi na wakawaita Wazee wa Ngwasuma kukamua siki ya Tuzo?Ni wazi wanajua ubora wa Bendi hiyo na kwa kiasi gani wacongo wameiteka sanaa yetu na kufunika kabisa…Kama mdau wa sanaa hapa Bongo kama Kepteni John Komba alimtuma Ally choki Congo kufuata Wanamuziki ili kukabiliana na ushindani wa hapa Bongo ni wazi kuwa kuwatoa Fm Academia kwenye Tuzo ni uamuzi wa kibaguzi na wa kukatisha tama wapenzi wa sanaa hapa Bongo….Ona hata katika Soka Timu kama Arsenal ya Uingereza ina wegeni karibu timu nzima na wala hata siku moja hujasikia chama cha mpira cha Uingereza au wadau wakisma kuwa eti wale ni wageni wasipewe sifa ambazo wanastahili kupata…Ndani ya Bendi ya FM Akademia kuna Watanzania wengi kama Josse Mara,Totoo Kalala,Levy Boy,Seif Mbonda na wengine wengi wanaofanya kazi sambamba na wengine ili kuwapa wapenzi burudani mahiri sasa kuwatenga katika hili ni uzandiki na Ubaguzi mbaya kama dhambi ya kula nyama ya mtu kama alivyosemaga Mwalimu Nyerere kuwa dhambi ya Ubaguzi huwa haiishi…
Eti kweli Tuzo hizi zina laana?najua utauliza kwanini?why why laana? Marehemu James Dandu alipofariki lilitokea zengwe sana la kugombea haki miliki ya kufanya tuzo hizi na hatimae Kilimanjaro wakapewa idhini hiyo na BASATA…wadau wakashauri kuwa ili kumuenzi mwasisi wa Tuzo hizi Marehemu James Dandu basi Tuzo hizi ziitwe Dandu Music Awards ili kuenzi wazo hili jipya aliloleta kijana Yule wa Mwanza nchini kwetu ili kukomboa muziki wetu na kuenzi kila mchango wa wana sanaa wa Tanzania.Waandaaji waende kutambika katika Kaburi la Dandu ili wafanye kazi wakiwa na Baraka za mwasisi ili kufanya kazi sahihi…laana haina dawa zaidi ya kukiri udhaifu na kuomba Baraka.Ni hayo tu mi ninayoyaona yatakayosaidia kupata njia wakati huu wa giza nene la Tuzo feki za Kili.
Kamati ya Kilimanjaro Awards na Wadhamini wafanye mjadala wa wazi na wadau wamuziki wetu ili kupata maoni na upata ushauri ili kunusuru Tuzo hizi ambazo zikifanywa vizuri zinasaidia kuijengea jina zuri la Kibiashara la Bia ya Kilimanjaro na Kuipa Heshima Kampuni ya Bia (TBL)

Ni hayo kwa leo,shukrani kwa wadau wote walionitumia maoni yao nikiwataja wachache haitakuwa mbaya …Gang Chomba wa Kibamba,simon wa Dodoma,Ashley wa Mwananyamala,Mr Kiwia wa Moshi,Riziki Minja wa babati- Arusha…Tupo pamoja Aluta Continua mpaka kieleweke!!!

Edwin Mac Temba
0715 000 890
m
mailto:mactemba2000@yahoo.com
www.mactemba.blogspot.com

No comments: