Tuesday, April 15, 2008

DIAMOND JUBILEE IWE FUNZO!!!

Juma nature na wanaume halisi wamedhihirisha wazi kuwa muziki kwao ni kazi na washabiki wanakubaliana na sanaa yao mpaka kuweza kuwafanya kuwapa ushindi wa Tatu bila,Mtazamo wangu upo wazi ni kuwa umewadia muda wa wasanii wetu kuwa makini na kufanya mambo ya msingi zaidi ya kukumbatia mambo yasio na muelekeo,mimi nilikuwa mmoja wa watu waliofurahishwa na kitendo cha Juma nature kujitoa katika himaya ya Said Fella,kwangu mimi kilikuwa ni kitendo cha ukomavu na ujasiri na kujiamini,Juma alikuwa anachukizwa na kitendo cha Fella kuwagawa wasanii wa Kundi la TMK Wanaume,Kuwagawa kwa maana kuna baaadhi ya wasanii walipewa msaada mkubwa wa kuandaa album zao na wengine kusahaulika na kuonekana kama hawana thamani katika kundi hilo.Kitendo hicho kilimfanya Juma Nature kujiona kama anawasaliti wenzake ambao walikuwa waasisi wa Kundi hilo kama Dollo,D-Chief,na wengine wengi...Nature ni tofauti na wasanii wengine wanaopenda ubinafsi na u mimi...Juma anapenda wasanii wengine nao wapate mafanikio kama yake ili iwe chachu wa chipukizi wengine kufuata nyayo zao,ndio maana anajitahidi sana kusaidia wanamuziki chipukizi ili kuweza kupata mafanikio katika sanaa yetu hii ya muziki...Kwangu mimi Juma nature ni mkombozi wa wasanii wachanga na wasio na sauti ya kutoa machungu yao...Jiulize Huyo Fella bila Juma Nature angejulikana lini katika solko letu la muziki???Wanaume Halisi ni mfano wa wapiganaji walioamua kudhihirisha kuwa wanaweza na wapo imara pamoja na kampeni zote mbaya wanazofanyiwa na baadhi ya watangazaji wasio na upeo wa muziki na wanaoendekeza njaa na tamaa,baada ya kupewa hela kidogo huanza kapmeni za kuwapaka matope...Hongera Juma Nature na Wanaume Halisi kwa kuwanyamazisha midomo wale wote wasio makini na wasiojua muziki huu ulitoka wapi...Huwezi kuitaja Temeke bila kumtaja Juma Kassim Kiroboto aka Sir Nature msanii pekee wa kizazi kipya aliyepata mafanikio makubwa hapa na nje ya nchi na kuweza kupata Tuzo nyingi hapa nchini na Hata nje ya mipaka ya nchi yetu...Kilichotokea Diamond Jubilee liwe kama funzo kwa mameneja kama Said Fella kuthamini kazi za wasanii wao,kupunguza kuwanyonya na kuhakikisha hawafanyi mambo yatawafanya washindwe kulinda makundi yao yasivunjike...Rafiki yangu Saleh Ally alitoa makala ya kuhusu mpambano huu na akasema baada ya mpambano huu kuna kundi moja litapata mafanikio na kupaa chati zaidi na moja litapotea kabisa katika ramani ya muziki wetu...hayo yameshadhihirika na ni kazi kwa Said Fella kujipanga na wenzake na kuamini Juma Nature sio mtu wa kawaida kwa maana Nyuma ya Juma Nature kuna maelfu ya wapenzi wa muziki na wanaompenda zaidi ya msanii yeyote wanayemjua wao...Yuko wapi King Crazy Gk na East Coast Team yake???Alianza bifu ya kitoto na Juma Nature mpaka mashabiki wakamdharau,akapoteza mvuto kwenye muziki,akawa anatupiwa cjupa na makopo jukwaani akiwa anafanya matamasha...hiyo ikamfanya apotee katika sanaa hii...So mtazamo wangu mimi ni tatu Bila na wamebana kisha wakaachia,Juma Nature mkombozi wa wanyonge kama Martin Luther King Jr

Ni hayo tu kwa leo na Big up sana kwa wapenzi wote wa Wanaume Halisi,wadhamini wa Show hiyo Mtandao wa kijanja tiGO,Kampuni bora ya bia Tanzania TBL kupitia bia yao bomba Kilimanjaro na Waandaji Prime Time Promotions chini ya Mkubwa Godfrey Kussaga...Congratulations sana!!!

1 comment:

Anonymous said...

sijui umeandika nini hapo juuu, huna jipya ila ni sifa za kijinga, ni ukweli ulio wazi waanaume halisi ni kundi la kichwa kimoja, bila ya nature hakuna kitu na nature mwenywewe hana nyimbo ya maana hata moja labda kipindi kile alipoimba HILI GAME wewe mwenyewe angalia hadi leo anateka watu na track hiyo sio mara sitaki demu album mzima amemuimbia demu. angalia upande mwingine wote vichwa acha temba, kuna chege, yp and y dash, mwenyewe kr mulla, jebi yaani balaa, na wote wana album zaidi ya moja hebu cheki halisi zaidi ya nature ni inspector wengine wote ni magalasha tuuuu. na huo ndio ukweli. kazi mipasho tuuu nyimbo zote mara 3 bila mara hakuna mwaka wa shetani mara ndege tunduni waambie washikaji zako waimbe nyimbo tofauti ya kuwaimba wenzaoqnqrdN