Saturday, November 24, 2007

TUZO FEKI ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS


Mac Temba,Edwin


Tuzo za muziki dunia nzima ni kipimo cha kazi nzuri pamoja na kioo cha mafanikio kwa mwanamuziki yeyote.Hapa kwetu Tanzania tuzo hizi zilianzishwa na Hayati James Dandu aka Mtoto wa Dandu,kuanzishwa kwa tuzo hizi kulileta changamoto kwa wasanii wetu na kupata faraja kuwa kazi zao zinathaminiwa.Kila kitu kina mapungufu yake lakini naamini kuwa watu hujifunza kutokana na makosa siku zote,lakini kwa waandaaji wa tuzo hizi wamepoteza muelekeo na kufanya tuzo hizo kupoteza mvuto pamoja na maana husika,Tuzo zimekuwa Tunzo na kuwa za kibiashara na kuwakatisha tamaa wanamuziki wanaofanya kazi kwa moyo wote na nguzu zote.Matatizo yamezidi mafanikio, na malalamishi yamezidi,kwa mtazamo wangu naona tuzo hizi ni feki na zipo kwa manufaa ya watu wachache wanaopata faida ya pesa za wadhamini wa Tuzo hizi.Unawezaje kupanga wasanii wasioimba aina moja ya muziki wagombanie tuzo moja?Je waandaji wanatumia vigezo gani?Napata mashaka kama kamati ya tuzo hizi kama wanajua muziki ni nini na madhara ya kuwapanga wasanii wachanga na wakubwa?Unawezaje kupanga muziki wa Taarab na Dansi kwenye kundi moja?Nilipata mshituko niliposikia eti wameweka Kaswida katika Tuzo za Muziki wa Tanzania mwaka huu?ni aibu kufanya kitu bila kupata ushauri.Kwa kuendelea hivi tuzo hizi zinapoteza muelekeo wa muziki wa Tanzania.Unawezaje kujua albamu hii ni bora bila kujua imeweza kuuza nakala ngapi sokoni?Unawezaje kumuweka mwanamuziki mwenye albamu moja kugombania tuzo ya mtunzi bora wa muziki?sioni maana ya kumuweka msanii mwenye albamu moja eti agombanie Tuzo ya mtunzi bora na mtunzi kama Hayati TX Moshi William?Huwezi kupata washindi wa tuzo kwa kupigiwa kura na wananchi eti kwa meseji za simu!!!,huwezi kupata washindi wa kweli.Ni wakati wa wanamuziki wa Tanzania kuamini kuwa Tuzo hizo ni feki na hazina maana katika muziki wetu.Kwani waandaji hawaoni mfumo unaotumika kupata washindi kwenye Kora au hata Tuzo kubwa duniani kama Grammy za marekani?Kuliko kutuletea tuzo za mizengwe kama hizi,Zinakera na kuwavunja nguvu wasanii wetu.Ni aibu kwa kampuni kubwa kama ya TBL kuendelea kudhamini Tuzo zilizopoteza muelekeo kama za Kilimanjaro Music Awards na kuharibu sura ya kibiashara ya Bia ya Kilimanjaro.

No comments: